Rwanda imelaani na kukanusha ripoti ya Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch kuhusu uchunguzi wake satellite unaonesha ongezeko la kaburi la kijeshi liliongezeka kwa ukubwa katika kipindi hiki cha mzozo wa mashariki ya DR Congo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baada kuchunguza picha hizo, Human Rights Watch imesema makaburi mpya 460 yameongezeka katika eneo la makaburi ya kijeshi kwenye Mji wa Kanombe jijini Kigali kati ya Disemba 15 na Julai 3.
Aidha, kwa mujibu ripoti yake iliyochapishwa kwenye mtandao wa X zinaonyesha mabadiliko kwenye eneo hilo la makamburi tangu mwaka wa 2022 ambapo makaburi mapya 1,171 yameongezeka.

Rwanda kwa upande wake imeendelea kusisitiza kwamba wanajeshi wake chini ya 10 ndio wameuawa katika mapigano ya hivi karibuni. Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo, ripoti hiyo ya HRW ni hatari na kwamba inapotosha.
Rwanda inatuhumiwa kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao wameteka Miji kadhaa ya mashariki ya DRC ikiwemo Goma na Bukavu.
Eneo la mashariki ya Congo lenye utajiri wa madini limekuwa likikabiliwa na mzozo wa zaidi ya miaka 30, pande zote hasimu kwenye mzozo huo zikituhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.