#HABARI: Burkina Faso inasema imeanzisha mfumo wa visa bila malipo kwa raia wa Afrika, kwa nia ya kuwezesha usafirishaji wa watu na bidhaa ndani ya nchi.
Uamuzi huo ulitolewa Alhamisi, wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri ulioongozwa na kiongozi wa kijeshi Kapteni Ibrahim Traoré
“Kuanzia sasa, raia yeyote kutoka nchi ya Kiafrika anayetaka kwenda Burkina Faso hatalipa kiasi chochote cha kulipia ada ya visa,” alisema Mahamadou Sana, Waziri wa usalama.
Kulingana na huduma ya habari ya serikali, kufuta ada ya visa kwa raia wa bara hilo, kunaonyesha kushikamana kwa Burkina Faso na maadili ya Kiafrika (Pan-Africanist), na kukuza ushirikiano wa kikanda.
“Mfumo huu wa viza bila malipo kwa raia wa Kiafrika pia utasaidia kukuza utalii na utamaduni wa Burkinafaso, na kuboresha taswira ya Burkina Faso nje ya nchi,” taarifa kutoka huduma ya serikali iliongeza.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania