
Mapigano ya hivi karibuni nchini Somalia hasa katika eneo linalojitawala la Jubaland, yanatishia musatakabali wa eneo hilo, hali ambayo imesababisha makundi ya kijihadi kama lile la Al-Shaabab kujipenyeza na kuongeza uwepo wake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kutokana na vita vya miaka nyingi nchini Somalia, baadhi ya majimbo kama vile Putland, Jubaland, Galmudung, Hirshabelle na Kusini Magharibi, yaliunda mifumo yake ya serikali kando na serikali kuu ya Mogadishu, ila misukosuko ya kisiasa katika jimbo la Jubaland inahatarisha usalama wa jimbo hilo, wadadisi wa mambo wakisema hili litawapa nguvu wapiganaji wa Alshabaab kuendeleza harakati zao.
Juma lililopita wanajeshi wawili wa serikali kuu ya Somalia waliuawa wakati wa makabiliano na wapiganaji watiifu kwa serikali ya Jubaland, katika eneo la Gedo ambalo linazozaniwa na serikali ya Mogadishu na ile ya Jubaland kutokana na ushawishi wa mji huo, wanajeshi wengine walikuwa wameuawa mwezi Julai.
Ni ubabe unaohusishwa na kiongozi wa jimbo la Jubaland, Ahmed Madobe na rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, wote wakilenga kudhibiti eneo hilo, Wawili hao ni mahasimu wa jadi kisiasa.
Vita kama hivi vimechangia magaidi wa Al-Shabaab, wenye uhusiano na kundi la Al-Qaeda, kuendelea kuchukuwa udhibiti wa miji muhimu nchini Somalia, wakati huu nchi hiyo ikijitayarisha kwa uchaguzi mwaka ujao.