
Israel imeidhinisha mradi mkubwa wa makazi katika eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu na walowezi wa Kiyahudi, uamuzi ambao jumuiya ya kimataifa imeonya kuwa unatishia uhai wa taifa la baadaye la Palestina.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Israel kwa muda mrefu imekuwa na nia ya kujenga makazi hayo mashariki mwa Mji wa Jerusalem, mipango yake ikionekana kukwama kutokana na pingamizi ya jamii ya kimataifa.
Tangazo la Israel limepingwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, anayesema hatua hiyo itagawa mara mbili ukingo wa Magharibi, hatua itakayotatiza juhudi zilizopigwa katika kulitambua taifa la Palestina.
Wiki iliopita, Waziri wa fedha wa Israel Bezalel Smotrich, aliunga mkono mpango wa kujenga karibia makazi 3,400 katika Ukingo wa Maghairbi.
Tangu mwaka wa 1967, makazi yote ya walowezi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi yametajwa kuwa ni haramu kwa mujibu wa sheria za kimataifa.