
Majaji nchini Ufaransa, wamegiza kufutwa kwa uchunguzi dhidi ya Agathe Habyarimana, mke wa aliyekuwa rais wa Rwanda Juvénal Habyarimana, anayedaiwa kuhusika kwenye mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nyaraka za Mahakama, zinaeleza kuwa Agathe Habyarimana, mwenye umri wa miaka 82, ambaye amekuwa akiishi Ufaransa tangu 1998, uwezo ni mkubwa sasa, hatafunguliwa mashtaka.
Hatua hii inakuja, licha ya Rwanda, mara kadhaa kuitaka Ufaransa, kumrudisha Agathe jijini Kigali ili kufunguliwa mashtaka.
Majaji hayo wamesema, hakuna ushahidi wa kutosha kuonesha kuwa alishiriki kwenye mpango wa kuwezesha mauaji hayo mabaya yaliyotokea Rwanda zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Aidha, Majaji hao wamesema, inavyoonekana Agathe, hakushiriki kwenye mauaji hayo, lakini alikuwa mwathiriwa mkubwa, kutokana na kifo cha mume wake, kaka yake na ndugu zake.
Uchunguzi dhidi yake, umekuwa ukiendelea tangu mwaka 2008 na kukamilika mwaka 2022, lakini viongozi wa mashtaka wanaopambana na ugaidi, waliomba uchunguzi mpya ambao ulitamatika mwezi Mei, bila ya kumfungulia mashtaka.