
Baada ya Rwanda, Eswatini na Sudan Kusini, ni zamu ya Kampala kufikia makubaliano kuhusu wahamiaji na serikali ya Marekani ya Donald Trump. Uganda, ambayo tayari inaongoza kwa kuwahifadhi wakimbizi barani Afrika ikiwa na zaidi ya wakimbizi milioni 1.7 katika ardhi yake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ndiyo nchi ya hivi punde zaidi barani humo kutangaza, siku ya Alhamisi hii, Agosti 21, kwamba imekubali kuwapokea wahamiaji waliotumwa na Washington chini ya baadhi ya masharti.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Kampala, Lucie Mouillaud
Kwa mujibu wa taarifa za Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, Vincent Bagiire, makubaliano yaliyofikiwa kati ya Washington na Kampala yanahusu raia wa nchi ya tatu “ambao huenda wasipewe hifadhi nchini Marekani” na wanasitasita au wana wasiwasi kuhusu kurejea katika nchi yao ya asili.
Hakuna takwimu zilizotolewa kwa idadi inayotarajiwa ya watu, lakini mpangilio ni “wa muda,” kulingana na Kampala, na masharti magumu kuhusu asili ya wahamiaji. Hakuna watoto ambao waliotengwa na familia zao au wanao na hatia za uhalifu, Katibu Mkuu anabainisha.
Wakati mnamo mwezi Julai 2025, Marekani iliwafukuza watu watano kutoka Asia na Karibiani na kuwatuma Eswatini, ambao utawala wa Trump uliwaelezea kama “wahalifu” walikataliwa kpokelewa na nchi zao. Uganda inapendelea watu waltakaohamishwa katiak ardji yake wawe Waafrika, taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa vyombo vya habari inaongeza, lakini masharti ya utekelezaji wa makubaliano hayo bado hayajachunguzwa.