Msimu wa mvua unaendelea nchini Niger, na kama kila mwaka, nchi hiyo inapata mvua kwa wiki kadhaa, mara kwa mara ikiambatana na mafuriko. Ingawa inadumu hadi mxezi Oktoba, idadi rasmi ya vifo iliyoripotiwa na mamlaka ni kubwa, na karibu vifo zaidi ya  hamsini hadi sasa, lakini idadi hii iko chini ya ile ya 2024, wakati mafuriko yalisababisha zaidi ya watu milioni 1.5 wasio na makazi

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwaka 2025, mafuriko yamesababisha vifo vya watu 47 na zaidi ya watu 56,000 wasio na makazi, kulingana na Kurugenzi Kuu ya polisi jamii. Mafuriko yaliathiri manispaa 78 kati ya 265 za nchi. Mamlaka imeanza kutoa msaada wa chakula, hasa kwa kusambaza nafaka.

Msimu wa mvua, hata hivyo, haujaisha, kwa ujumla hudumu hadi mwezi Oktoba. Kwa hivyo, tahadhari inabaki kuwa muhimu.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, maafisa wa kikosi cha zima moto nchini Niger walitoa ukumbusho wa baadhi ya hatua za usalama zinaopaswa kuzingatiwa: musikae katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko, katika makazi hatarishi au tete, na haswa msivuke mito au kujificha chini ya miti.

Niger inakabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi na ilishuhudia msimu wa mkali wa mvua mwaka jana. Mafuriko hayo yalisababisha vifo vya takriban watu 400 na zaidi ya watu milioni 1.5 wasio na makazi katika mikoa minane ya nchi, pamoja na kuharibu mazao na mifugo.

Msikiti wa zaidi ya miaka 200 pia uliporomoka huko Zinder. Mamlaka ilibidi kuahirisha kuanza kwa mwaka wa shule kwa mwezi mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *