#HABARI: Baadhi ya Wakulima wanaojishughulisha na Kilimo cha Tumbaku katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wameishukuru serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wanunuzi wa zao hilo ambapo siku za nyuma walisimama kwenye uzalishaji wa zao hilo kwa kukosa wanunuzi na kusababisha kuwa na maisha magumu zaidi.
Kujitokeza kwa wanunuzi wa zao la Tumbaku ikiwemo Kampuni hii ya Premium Active Tanzania, katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, kumeleta faraja kubwa mno kwa wakulima ambao wanaeleza hisia zao walivyoathirika walipokosa wanunuzi wa zao hilo.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania