#HABARI:Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekanusha taarifa zinazodai kuwa mfumo wake wa uchaguzi umeunganishwa na mifumo y…#HABARI:Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekanusha taarifa zinazodai kuwa mfumo wake wa uchaguzi umeunganishwa na mifumo y…

#HABARI:Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekanusha taarifa zinazodai kuwa mfumo wake wa uchaguzi umeunganishwa na mifumo ya NIDA ama chama cha siasa na kwamba uchaguzi tayari umekamilika.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima, amesema taarifa hizo ni za uongo na upotoshaji unaolenga kuibua taharuki kwa wananchi huku akibainisha kuwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijaunganishwa na mfumo wowote wa serikali au taasisi binafsi kwa ajili ya uchaguzi.

Kailima amebainisha kuwa mfumo wa kupiga kura nchini, kuhesabu kura na kutangaza matokeo, hautumii teknolojia ya Kielektroniki, bali ni wa kawaida (Manual), na vyama vya siasa vilishakabidhiwa nakala za Daftari la Wapiga Kura ili kuwawezesha mawakala wao kutambua wapiga kura siku ya uchaguzi.

Kailima amewataka wananchi na wadau wa uchaguzi kuupuuza upotoshaji huu kwani taarifa zote sahihi kuhusu uchaguzi zinapatikana kwenye tovuti na kurasa rasmi za INEC, hivyo amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa kuzingatia kauli mbiu yake ‘Kura Yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura’ kweye Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *