Photos from ITV Tanzania’s postPhotos from ITV Tanzania’s post

#HABARI: Wakili na Mwanaharakati wa Haki za kijamii, Mwanaisha Mndeme, amejitokeza kuchukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni, kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, zoezi hilo limefanyika katika Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Jijini Dar es Salaa.

Baada ya kuchukua fomu, Wakili Mwanaisha amesema ameamua kugombea kwa dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Kigamboni na kuhakikisha sauti yao inasikika Bungeni na kubainisha kwamba moja ya vipaumbele vyake ni kuhakikisha barabara katika Jimbo hilo zinaboreshwa ili kuondoa usumbufu kwa wananchi, pia kuboreshwa kwa huduma za vivuko, ili ziwe za uhakika na nafuu kwa wananchi wanaotegemea usafiri huo kila siku.

Mwanaisha ameweka wazi kuwa atapigania kupunguzwa kwa ada ya Daraja la Mwalimu Nyerere, akieleza kuwa daraja hilo lilipaswa kuwa mkombozi kwa wakazi wa Kigamboni, lakini ada yake imekuwa mzigo mkubwa kwao, amewaomba wananchi wa Kigamboni kushirikiana naye kupitia ACT-Wazalendo ili kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa wote.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *