#HABARI: Aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM, Jokate Mwegelo amemshukuru Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa imani yake kubwa kwake ikiwemo kumpendekeza na kisha kuteuliwa na Halmashauri kuu ya CCM Taifa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM mpaka jana majukumu yake yalivyokoma na ameahidi ataendelea kuilinda imani hiyo kwa wivu mkubwa sana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jokate amesema “Umeweka alama kubwa kwenye maisha na historia yangu ya uongozi kwa kunipa nafasi ya kutumikia jumuiya mbili kubwa za CCM, UWT na hii ya Vijana, nawashukuru Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti Bara Stephan Masato Wasira-Bara kwa miongozo yenu mizuri kwangu na kwa UVCCM kwa ujumla”
“Nakushukuru Dkt. Balozi Emmanuel John Nchimbi Katibu Mkuu Wa CCM Mstaafu na Mgombea Mwenza kwa malezi na maelekezo yako ya kiuongozi na kiutendaji kwa kweli mengi nimejifunza chini ya usimamizi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM-Taifa, nishukuru Wajumbe Wote wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa, Kamati Maalum na Jumuiya zote za CCM kwa ushirikiano mkubwa mlionipa katika utekelezaji wa majukumu yangu nikiwa katibu mkuu wa UVCCM”
“Kwa umaalumu wake Naushukuru Umoja wa Vijana wa CCM kwa ngazi zote, kipeke Baraza kuu la UVCCM Taifa, Kamati ya Utekelezaji, Sekretariat ya Baraza Kuu La Uvccm Taifa chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wetu Bingwa CDE Kawaida kwa upendo na ushirikiano mkubwa mlionipa katika utekelezaji wa majukumu yangu nikiwa Katibu Mkuu wa UVCCM, bila nyinyi nisingeweza kuyatekeleza Nawashukuru sana sana sana, nawapenda mnooooo”
“Nitumie fursa hii kumpongeza na kumtakia kila la kheri Katibu Mkuu mpya wa UVCCM Ndugu yangu Khalid Mwinyi kwa imani hii, Wishing you nothing but the very best, uwezo wako ni mkubwa, Mwenyezi Mungu akutangulie. Amiiiin 🙏🏽
“Nawashukuru VIJANA WOTE nchini kwa ushirikiano wenu kwangu katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yangu”