
Miaka minne baada ya moto kuzuka katika Hifadhi ya Kibinafsi ya Lolldaiga kufuatia ajali wakati wa mafunzo na Jeshi la Uingereza, ambalo lina kambi katika eneo hilo, Uingereza imekubali kulipa pauni milioni 2.9 kwa watu 7,700 waliokumbwa na athari za moto huo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Albane Thirouard
Huu ni mwisho wa vita vya kisheria vilivyodumu kwa miaka minne nchini Kenya. Katikati mwa nchi, zaidi ya watu 7,700 wamepokea tu pauni milioni 2.9 kutoka kwa serikali ya Uingereza kama fidia ya moto uliozuka mnamo mwaka 2021 katika Hifadhi ya Kibinafsi ya Lolldaiga.
Kufuatia ajali wakati wa mafunzo ya vikosi vya kijeshi vya Uingereza, ambavyo vina kambi ya mafunzo katika eneo la Nanyuki, heka 2,800 za mimea zilifuka moshi. Maafa hayo pia yalisababisha uharibifu mkubwa kwa mifugo, mazao, mali na afya za watu wanaoshi karibu na hifadhi hiyo.
Suluhu kati ya pande husika
Miaka minne baadaye, wahasiriwa hatimaye wamefikia makubaliano ya amani na London ili kupata fidia. Malipo ya kwanza ya fidia yalianza wiki hii, kulingana na Kelvin Kubai, wakili aliyewatetea, ambaye anabainisha kuwa “matokeo haya ni bora zaidi ambayo tungeweza kutarajia, kutokana na mazingira. Njia mbadala ingekuwa kuendeleza kesi kwa karibu miaka minane, ambayo haingekuwa na ufanisi katika suala la muda na gharama kubwa kwa walalamikaji wengi.”
Ameongeza: “Ninaona hii kama hatua katika mwelekeo sahihi. Wakati moto ulitokea huko Lolldaiga huko nyuma, ukweli kwamba Uingereza imekubali kulipa fidia kwa hii inaonyesha kwamba inaanza kusikiliza wakati baadhi ya matendo yake yanakiuka haki za mazingira za wakazi wa eneo hilo.”
Wakati maelfu kadhaa ya wanajeshi wa Uingereza wakiendelea kuja Nanyuki kila mwaka, uwepo wao unazidi kuleta utata nchini Kenya. Wanashutumiwa haswa kwa ukiukaji wa haki za binadamu, ambao kwa sasa suala hili linafanyiwa uchunguzi na bunge nchini Kenya.