Kwa mujibu wa Burt, Gaza kwa sasa ni “jinamizi la kiusalama” kwa chombo chochote cha kusimamia. Ukanda huo, amesema, umejaa magenge, silaha, na uhalifu.
“Kazi ya kwanza itakuwa ni kuzuia uporaji, kuondoa silaha mikononi mwa raia, na kurejesha hali ya kawaida. Hili linaweza kuchukua muongo kutekelezwa ipasavyo.”
