Hali ya utulivu kwa sasa inatawala huko El-Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, mji pekee katika jimbo hilo ulio chini ya udhibiti wa jeshi. Mapigano makali yameendelea kwa siku tisa mfululizo. Wanajeshi kutoka Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) wamelenga maeneo ya kimkakati katika jiji na kwa mara nyingine wamejaribu kusonga mbele bila mafanikio. RSF wanahangaishwa na udhibiti wa mji wa El-Fasher licha ya kuzingirwa na njaa kwa zaidi ya miezi 16, huku wakaazi 300,000 wakisalia huko.
