
Mali, Burkinafaso na Niger, ambazo zote zipo chini ya uongozi wa kijeshi, zilijiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS, mwezi Januari baada ya kuunda muungano wao wa pamojawa nchi za Sahel, AES wakati wakipambana na uasi wa muda mrefu wa wapiganaji walio na itikadi kali.
Mkutano huo utakaomalizika Jumatano umetajwa na serikali ya Nigeria kuwa wa kwanza mkubwa kuwahi kufanyika barani Afrika na umewaleta pamoja maafisa wa ngazi za juu jeshini kutoka mataifa mbali mbali ya bara hilo kujadili juu ya mikakati ya pamoja na kutafuta suluhisho kuhusu mahitaji ya kiulinzi ya bara la Afrika.
Akizungumzia changamoto za usalama ambazo “hazitambui mipaka”, Mkuu wa jeshi la Nigeria Christopher Musa alitoa wito wa “usanifu mpya wa ushirikiano wa usalama unaoongozwa na Afrika”. Mkutano huo ulioanza jana (25.08.2025), unatarajiwa kukamilika kesho Jumatano (27.08.2025).
Niger na Nigeria zimekuwa zikikabiliana na changamoto katika ushirikiano wa kijeshi katika vita vyao dhidi ya kundi la Boko Haram na kundi linalojiita dola la kiislamu katika mkoa wa Afrika Magharibi wanaotekeleza uasi katika maeneo ya mipakani.
Uhusiano kati ya mataifa hayo na jirani zake wa AfrikaMuungano wa AES waingia kwenye mvutano wa kidiplomasia na Algeria Magharibi uliingia doa mwaka 2023 baada ya mapinduzi wa kijeshi wakati ECOWAS ilipoiwekea Niger vikwazo, na chini ya uongozi wa Jumuiya hiyo inayosimamiwa na Nigeria katika urais wa kupokezana, ilitishia kuichukulia hatua za kijeshi iwapo haitorejesha uongozi wa kiraia kwa kiongozi aliyepinduliwa Mohamed Bazoum.
Niger, Mali na Burkina Faso zimeshuhudia ushirikiano wao wa kijeshi ukikwama na majirani zao kama Benin, inayojaribu kuyadhibiti mashambulizi ya makundi yenye silaha ya Sahel.