#HABARI: Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mafia mkoani Pwani Bwana Salehe Kikweo amefariki dunia asubuhi ya leo wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni.
Akithibitisha kutokea kwa kifo cha katibu huyo ambae pia alishafanya kazi huko wilayani Handeni, Katibu wa sasa wa chama hicho Handeni Bi. Mayasa Kimbau amesema kifo hicho wamekipokea kwa masikitiko makubwa kwani siku ya jana walikua naye hadi majira ya jioni.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Handeni, Amiri Changogo amesema mara ya mwisho aliongea na marehemu usiku wa jana na kudai kuwa anajisikia kuumwa ambapo alimshauri afike hospitali ili kwenda kupata matibabu hata hivyo pamoja na jitihada za madaktari kuokoa maisha ya Bwana Kikweo zilishindikana na hatimaye kufariki dunia.
Bi Mayasa Kimbau ambaye ni Katibu wa CCM wilayani hapo amesema taratibu za mazishi zinaendelea wilayani hapo ambapo marehemu ndipo alipozaliwa na kukulia kabla hajajiunga na CCM.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania