#HABARI: Kufuatia mauaji ya Mlinzi wa Soko la Ussoke, lililopo Wilaya ya Urambo mkoani wa Tabora, Bw. Nasoro Mgalula, aliyeuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Agosti 18. 2025, wakati walipokuwa wakitaka kuiba mali na fedha zilizopo kwenye maduka ya soko hilo Afisa wa Jeshi la Polisi SP. Dorick Mipango, ameonekana akiwahubiria wakazi wa Kata hiyo juu ya umuhimu wa kutofumbia macho matukio hayo.
Wakati hayo yakiendelea tayari vyombo vya usalama Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Urambo vinaendelea na msako wa kuwatafuta wahusika wa tukio hilo.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania