#HABARI: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw#HABARI: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw

#HABARI: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw. Kakulu Burchad Kakulu, amechukua fomu katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Bw. Kakulu amesema kuwa CCM imefanikiwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa ahadi zilizomo katika Ilani ya Uchaguzi, jambo linalotoa matumaini makubwa ya ushindi kwa chama hicho, hususani katika Jimbo la Mbagala.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *