#HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Bi Irene Mlola, amewataka wakulima nchini kuacha mara moja tabia ya kuuza mazao yao nje ya mfumo rasmi uliowekwa na serikali, akisisitiza kuwa njia hiyo huwanyima faida stahiki na kuharibu mnyororo wa thamani wa mazao.
Bi Irene Mlola amesema serikali imeweka mifumo bora na rafiki kwa mkulima, ukiwemo mfumo wa Stakabadhi za Ghalani na minada ya kidijitali, ili kuhakikisha kuwa mkulima anapata bei nzuri, usalama wa mazao, pamoja na soko la uhakika.
Katika kijiji cha Manawa, Kata ya Misasi, wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza baadhi ya wakulima wameipongeza serikali kwa kuanzisha mfumo huu wa mauzo kupitia stakabadhi ghalani.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania