Chanzo cha picha, Getty Images
Katika mwaka uliotawaliwa na na migogoro, mataifa matano yameendelea kuorodheshwa miongoni mwa mataifa yenye amani zaidi duniani. Wakazi wamefichua jinsi sera na utamaduni vinavyoyafanya maisha yao ya kila siku kuwa ya hali ya utulivu.
Katika mwaka 2025 amani inaweza kuonekana kama jambo adimu kutokana na kuongezeka kwa vita vya kimataifa, kuimarishwa kwa usalama wa mipaka unaimarishwa ya nchi , na mvutano wa kibiashara unaoendelea kuongezeka duniani.
Kulingana na Ripoti ya Amani ya Dunia ya 2025 (GPI), idadi ya migogoro ya kanda imefikia kiwango chake cha juu zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia, na migogoro mingine mitatu iliibuka mwaka huu pekee. Nchi nyingi zinajibu kwa kuimarisha majeshi yake.
Hata hivyo licha ya takwimu hizo za kutisha, baadhi ya mataifa yanaendelea kutanguliza amani.
Taasisi ya Uchumi na Amani , inafuatilia viashiria 23, kuanzia migogoro ya nje na matumizi ya kijeshi hadi hatua za usalama kama vile ugaidi na mauaji.
Nchi zilizoorodheshwa katika kiwango hiki zimekuwa na msimamo thabiti kwa takriban miongo miwili, na kuonyesha utulivu ambao sera za amani zinaweza kuuleta kwa muda mrefu.
Tulizungumza na wakazi katika baadhi ya nchi zenye amani zaidi duniani ili kujifunza kuhusu jinsi sera hizo zinavyounda maisha yao ya kila siku – na kinachowapa hali ya kipekee ya usalama na utulivu.
Iceland
Ikiorodheshwa kuwa nchi nambari moja tangu 2008, Iceland inasalia kuwa taifa lenye amani zaidi duniani, linaloongoza katika nyanja zote tatu: usalama amani na tulivu. Hata ilirekodi uboreshaji wa 2% mwaka huu, na kuongeza pengo kutoka kwa nchi iliyoshika nafasi ya pili kwenye orodha.
Kwa wenyeji, hali hiyo ya usalama inashuhudiwa katika maisha ya kila siku. “Ingawa hali mbaya ya hewa, hasa wakati wa msimu wa baridi, inaweza isilete hali ya utulivu kila wakati, jamii bado inaweza kuwa na usalama,” alisema Inga Rós Antoníusdóttir, aliyezaliwa Iceland na ni meneja mkuu wa Intrepid Travel Ulaya Kaskazini .
“Unaweza kutembea peke yako usiku mara nyingi bila wasiwasi; utaona watoto wakilala kwa amani nje ya mikahawa na maduka huku wazazi wao wakifurahia mlo au [wanafanya] shughuli zao ; na polisi wa eneo hilo hawabebi bunduki.”
Chanzo cha picha, Getty Images
Inga anasema hii inatokana na sera za usawa wa kijinsia zinazoongoza duniani kwa kuwaruhusu wanawake kujisikia salama. “Fursa sawa na mifumo thabiti ya kijamii inaunda jamii ya haki na salama kwa kila mtu,” alisema.
Anapendekeza wageni wapate utulivu huu wa ndani kwa kujiunga na wenyeji katika mila za kila siku. “Nenda kuogelea kwenye kidimbwi cha maji yenye jotoardhi na uzungumze na watu usiowajua ndani ya maji moto; panda mlima, iwe ni alasiri kupanda Mlima Esja nje ya Reykjavik au safari ya siku nyingi katika nyanda za juu,” alisema. “Iceland halisi iina muziki na sanaa yake inayostawi, kwa asili mbali na na katika kila aina ya hali ya hewa.”
Ireland
Ingawa iliangaziwa na mizozo mwishoni mwa Karne ya 20, Ireland ya leo inaendelea kuweka amani mbele. Ilipata alama za juu zaidi kwa kupunguza upiganaji wake mwaka baada ya mwaka na kuorodheshwa kama mojawapo ya nchi zilizo na migogoro michache zaidi inayoendelea ya ndani na kimataifa. Pia iliweka kati ya 10 bora kwa usalama na usalama wa jamii, na mitazamo ya chini ya uhalifu na vurugu.
”Watu wanawajali wengine hapa. Ni aina ya mahali ambapo unaweza kumuuliza mtu usiyemjua msaada na atakufanyia kazi” – Jack Fitzsimons
Hisia hiyo inaenea kote nchini kwa wakazi. “Hisia ya kina ya maiasha ya ushirikiano na urafiki inakufanya ujisikie umekaribishwa na umestarehe, iwe uko katika mji mdogo au jiji kubwa,” alisema Jack Fitzsimons, mkazi wa Kildare na mkurugenzi wa uzoefu katika Kasri la Kilkea . Anagundua kuwa mifumo dhabiti ya usaidizi wa kijamii na kuzingatia ustawi wa jamii pia hupunguza ukosefu wa usawa na mvutano. “Watu wanawajali wengine hapa,” aliongeza. “Ni aina ya mahali ambapo unaweza kumuomba mtu asiyemjua msaada na watatoka nje kwa ajili yako.”
Katika hatua ya kimataifa, nchi inadumisha kutoegemea upande wowote kijeshi (ambayo inaizuia kuwa mwanachama rasmi wa Nato, mojawapo ya nchi nne tu za Ulaya bila uanachama), na upendeleo wa kutumia diplomasia kutatua migogoro. Nyumbani, nchi inatanguliza uhifadhi wa mandhari na maeneo yake ya kitamaduni, na inahakikisha wasafiri daima wanahisi kukaribishwa. “Bado inanishangaza jinsi wageni wanavyoshangaa kuhusu jinsi watu wa Ireland walivyo wa kirafiki. Kwetu sisi, ni sehemu tu ya kitambaa chetu, kwani tuna hisia ya ndani ya ukarimu kwa wageni wa ng’ambo,” Fitzsimons alisema.
Chanzo cha picha, Getty Images
Hali ya utulivu ya Ireland pia husababisha hali ya amani. “Kamwe hauko mbali na kasri, matembezi tulivu ya msituni au kikao cha muziki cha kitamaduni katika baa ya kupendeza,” Fitzsimons alisema. “Maisha yanasonga kwa kasi zaidi hapa, na watu bado wanathamini mazungumzo na hadithi. Uhusiano huo wa kibinadamu unaonekana wazi.”
New Zealand
Mwaka huu New Zealand ilipanda nafasi mbili nakufikia hadi nambari tatu, kutokana na kuboreshwa kwa utulivu na usalama pamoja na kuwa na maandamano machache na athari zinazohusiana na ugaidi.
Kama taifa la kisiwa katika Pasifiki, jiografia ya New Zealand inaipa ulinzi wa asili dhidi ya migogoro ya nje, lakini sera zake za ndani pia zinawapa wakazi hisia ya amani. “Sheria za bunduki za New Zealand ni miongoni mwa sheria kali zaidi duniani, ambazo huchangia kabisa hali ya usalama,” alisema Kiwi Mischa Mannix-Opie, mkurugenzi wa uzoefu wa wateja katika kampuni ya uhamishaji ya Greener Pastures.
Anabainisha kuwa ni mahali ambapo watoto hutembea kuelekea shuleni, watu huacha milango yao ikiwa haijafungwa na wenye magari husimama ili kusaidia ikiwa gari limeharibika kando ya barabara. “Kuna imani ya jumla kwa wengine na katika mifumo inayokuzunguka, ambayo inajenga hisia halisi ya jumuiya katika maisha ya kila siku.”
Zaidi ya mtandao thabiti wa usalama wa kijamii na ufikiaji wa huduma ya afya kwa wote, watu wa New Zealand wanathamini uhusiano wao na asili, iwe ni kutembea ufukweni, kupanda msituni au kuwa na glasi ya divai chini ya nyota, anasema Mannix-Opie.
Maana ya jumuiya pia inamaanisha sherehe na matukio mengi kwa umri wote, kwa kusisitiza mazingira yanayofaa familia. Ingawa wageni wengi huja kwa mandhari, mara nyingi ni hisia ya usalama na ushiriki katika jumuiya ambayo huacha hisia ya kudumu.
Chanzo cha picha, Getty Images
“Zaidi ya kuwa na mandhari ya kadi ya posta, New Zealand ina mengi mazuri zaidi. Watu ni wakweli, utamaduni wa Wamaori wenye mvuto unapatikana kila wakati na unaweza kubadilisha mtazamo wako,” Mannix-Opie alisema. “Mteja mmoja aliniambia kuwa ingawa New Zealand ni nzuri, ni watu wetu ambao ndio nguvu zetu kuu.”
Austria
Austria ilishuka nafasi moja mwaka huu hadi ya nne lakini bado imeorodheshwa juu katika viwango vyote. Kama Ireland, Austria inakubali sera iliyoidhinishwa kikatiba ya kutoegemea upande wowote, na kuizuia kujiunga na muungano wa kijeshi kama Nato. Hili huwezesha nchi kuzingatia umakini na rasilimali zake ndani.
Nchi 10 bora kulingana na kipimo cha viwango vya amani ya duniani ya 2025
“Sera ya miongo mingi ya Austria ya kutoegemea upande wowote ina maana kwamba taifa linawekeza kwa watu wake badala ya migogoro,” alisema Armin Pfurtscheller, mmiliki wa SPA-Hotel Jagdhof . “Mtandao dhabiti wa usalama wa kijamii, huduma ya afya ya kiwango cha kimataifa na elimu bora huleta utulivu na uaminifu.”
Neustift anaishi katika Bonde la Stubai, ambako anasema watu wanazurura kando ya Mto Ruetz usiku wa manane, nyumba huachwa bila kufungwa na baiskeli hukaa bila minyororo nje ya mikahawa. “Salama sio tu takwimu, ni jinsi maisha yanavyohisi.”
Pfurtscheller pia anaona hali hii ya urahisi kati ya wageni wanaokuja kukaa kwenye bonde. “Baada ya siku kadhaa, mabega yao yanashuka, msongo wa mawazo unayeyuka, na wanalala kama walivyokuwa watoto,” alisema. “Wanaanza kuona sauti ya mto, jinsi mwanga unavyobadilika kwenye milima na furaha rahisi ya kupumua kwa kina. Hiyo ndiyo hisia kuu ya usalama inayotolewa na mahali hapa: uhakika kwamba hapa, uko huru kuwa.”
Singapore
Ikidumisha nafasi yake katika nambari sita, Singapore ndio nchi pekee ya Asia katika 10 bora (Japani na Malaysia zikija katika nafasi za 12 na 13, mtawalia). Inashika nafasi ya juu zaidi kwa usalama na usalama, hata wakati inadumisha moja ya viwango vya juu zaidi vya matumizi ya kijeshi kwa kila mtu, ikizidiwa na Korea Kaskazini na Qatar pekee.
Chanzo cha picha, Getty Images
Ukosefu wa migogoro inayoendelea na usalama wa ndani husababisha hisia kubwa za usalama kwa wakazi wengi. “Mimi hutembea usiku sana na sihisi uoga.
Kutembea kwenda nyumbani hakulemei wala hakuleti wasiwasi kama ilivyo katika miji mikubwa ya mijini,” alisema mkazi Xinrun Han. “Kuna faraja ya 100% na kuaminiana katika mfumo, ambayo hufanya mazingira kuwa ya utulivu, kujali na amani.”
Ingawa msimamo wa Singapore kuhusu ulinzi wa LGBT+ unaweka mipaka ya uhuru fulani, ndoa za watu wa jinsia moja bado haziruhusiwi, maendeleo ya kijamii yanaonekana kupitia matukio kama vile tamasha inayokua ya fahari ya Pink Dot . Wengi waliripoti kujisikia salama katika mkutano huo mwaka huu kuliko katika miongo iliyopita huku vijana wa Singapore wakishinikiza kukubalika zaidi.
Han anapendekeza wageni kukumbatia uhuru unaokuja na usalama, kama vile kutembea kando ya mto saa 02:00, kunyakua kitu kutoka kwa muuzaji wa chakula cha usiku wa manane au kutembelea bustani baada ya giza kuingia. “Inajisikia huru sana, iwe wewe ni mkazi au unatembelea tu.”