s

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika kile kinachoonekana kama mwendelezo wa sera za kulinda uchumi wa ndani, Serikali ya Tanzania imetangaza rasmi marufuku dhidi ya shughuli 15 za kibiashara kwa raia wa kigeni.

Amri hii imezua hisia kali ndani na nje ya mipaka ya taifa hilo hasa kwenye mitandao ya kijamii, huku maswali mengi yakiibuka kuhusu malengo yake halisi. Ingawa waraka wa serikali haukutaja nchi yoyote, mjadala mkubwa umezuka nchini Kenya, ambako hisia za “kulengwa” na hatua hiyo zimeibuka.

Kwa upande wa Tanzania, serikali inasema hatua hiyo imelenga kulinda fursa za ajira, kipato na uwekezaji kwa wananchi wake hasa wale wanaojihusisha na biashara ndogondogo.

Lakini kwa upande mwingine, baadhi ya wanasiasa na wadau wa biashara wa Kenya wanasema wazi kuwa wameguswa moja kwa moja, wakiona huu kama mwendelezo wa kile wanachokiita “mtazamo wa kisiasa usio rafiki” kutoka kwa jirani yao wa kusini.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *