
Nchini Kenya, wahifadhi wa Hifadhi ya Mazingira ya Tsavo, mashariki mwa nchi, wana wasiwasi. Tsavo, inayoundwa na hifadhi 35, ni mojawapo ya hifadhi kubwa zaidi za asili barani Afrika. Kusitisha kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) mwezi Januari 2025 kunahatarisha mipango yake ya uhifadhi, na hivyo kuhatarisha kuzuka upya kwa ujangili na migogoro ya ardhi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaƫlle Laleix
Katikati ya Hifadhi ya Tsavo, nchini Kenya, wakulima 80 wanatarajia kuwa wafugaji nyuki hivi karibuni. Lakini baada ya mwaka wa mafunzo, bado wanasubiri mizinga 1,200 ambayo itawawezesha kujiongezea kipato. Agizo hilo lilitupiliwa mbali kwa sababu ya ukosefu wa fedha.
Kulingana na Jumuiya ya Hifadhi za Mazingira ya Taita Taveta, kutokana na mpango wa USAID, zaidi ya wakazi 1,500 wa Tsavo wamejifunza mbinu za kilimo kiikolojia, walinzi 133 wamepewa mafunzo, na migogoro kati ya wakulima na wanyamapori imepungua kwa 90% katika miaka miwili. Haya yote ni mafanikio ambayo kusitihwa kwa ufadhili wa USAID kunaweza kuhatarisha na kusababisha hali kuwa ngumu. Shirika hilo la Marekani lilikuwa limeahidi zaidi ya dola milioni 2 kwa mradi unaoendelea hadi 2027.
“Leo, tunazingatia miundo mingine ya ufadhili kama vile mikopo ya kaboni au mikopo ya viumbe hai,” anaeleza Alfred Mwanake, mkuu wa Muungano wa Hifadhi za Mazingira za Taita Taveta.
Kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani kunakuja wakati Kenya imejitolea kurejesha zaidi ya heka milioni 5 ili kuunda hifadhi za asili. Kulingana na kampuni ya ushauri ya Andersen, nchini Kenya, ruzuku za Marekani ni karibu 3% ya matumizi ya umma nchini humo.