
Nchini Mali, Mei mwaka jana, kwa agizo la rais, utawala wa kijeshi ulifuta baadhi ya vyama 297 vya kisiasa. Vyama vya siasa hasa vya upinzani vilianzisha mashauri ya kisheria kupitia mawakili ili uamuzi huu ubatilishwe. siku ya Jumatatu, Agosti 25, Mahakama Kuu ya JWilaya ya 1 imetoa uamuzi wake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa kanda, Serge Daniel
Kinyume na maamuzi ya awali ya mahakama, Mahakama Kuu ya Wilaya ya 1 huko Bamako, Mali, imetangaza kukubali malalamiko yaliyowasilishwa na kundi la mawakili. Ombi la kubatilisha ufutaji wa vyama vyote vya siasa sasa liko mezani kisheria.
Habari Nyingine: mahakama imeamua kwamba kabla ya kutoa uamuzi juu ya uhalali wa kesi hiyo, mapitio ya awali ya uhalali wa katiba ya amri zinazopingwa inahitajika. Kwa hivyo kesi katika hatua ya awali inapelekwa kwa Mahakama ya Katiba.
Uamuzi huu wa Mahakama Kuu ya Wilaya ya 1 ya Bamako hausemi kwa uthabiti agizo za kufuta vyama vya kisiasa, lakini unaviweka katika tishio la uwezekano wa kubatilishwa mara tu Mahakama ya Juu itakapotoa uamuzi juu ya utii wao wa kikatiba.
Katika taarifa, mmoja wa mawakili wa walalamikaji, Bw. Mountaga Tall—yeye ambaye sasa ni mwanachama wa upinzani—anabainisha kwamba Majaji tisa wana fursa ya kihistoria ya kuthibitisha kwamba Mahakama ya Kikatiba ndiyo mlinzi wa uhuru na uhalali wa jamhuri.
Kwa upande wake, vuguvugu la Patriotic Resistance Front (RPF), linaloundwa na wapinzani walio uhamishoni kwa kulazimishwa, linatoa wito, katika taarifa, “kuwa macho na kuendeleza uhamasishaji,” kabla ya kuongeza kwamba “Mali itarejea tu kwenye njia ya uhuru na heshima kwa kuondoka kwa utawala wa kijeshi.”