Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea imekubali kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Senegal mwenye umri wa miaka 24 Nicolas Jackson kwenda Bayern Munich. (Bild)
Kiungo wa England Kobbie Mainoo, 20, atafikiria kuondoka Manchester United katika wiki ya mwisho ya dirisha la usajili iwapo klabu itapokea ofa inayofaa. (Talksport)
Crystal Palace wamewasilisha ofa ya pauni milioni 15 kwa ajili ya kumnunua beki wa Uswizi wa Manchester City Manuel Akanji, 30. (Sun)
Mshambuliaji wa Denmark wa Manchester United Rasmus Hojlund, 22, atapata ongezeko kubwa la mshahara iwapo atakubali kujiunga na Napoli kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Gazzetta dello Sport)
Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham wanaweza kukosa mchezaji wa nne baada ya Como kukataa ofa ya pauni milioni 50 kutoka Spurs kwa ajili ya kiungo wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 Nico Paz. (Mirror)
Wolves watampa mshambuliaji Jorgen Strand Larsen mkataba mpya baada ya kukataa ofa ya pauni milioni 50 kutoka Newcastle lakini bado wanaweza kushawishika kumuuza mshambuliaji huyo wa Norway mwenye umri wa miaka 25 iwapo watapokea dau la zaidi ya pauni milioni 75. (Telegraph)
Strand Larsen anatamani kujiunga na Newcastle huku Magpies wakipanga kuwasilisha ofa nyingine, lakini haonekani kama mbadala wa mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, ambaye anawindwa na Liverpool. (The I)
Maofisa wa Newcastle, akiwemo mmiliki mwenza Jamie Reuben, wamezungumza na Isak nyumbani kwake kwa lengo la kumshawishi abaki klabuni na kurejea kwenye kikosi cha Eddie Howe licha ya kuwaniwa na Liverpool. (Daily Mail),
Chanzo cha picha, Getty Image
Kocha wa Wolves Vitor Pereira anatamani kumsajili beki wa kati wa Girona Ladislav Krejci, 26, na wachezaji wengine nafasi ua kiungo wa kati na mshambuliaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi kabla ya dirisha kufungwa. (Guardian)
Borussia Dortmund wako karibu kufikia makubaliano na Wolves kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Kireno mwenye umri wa miaka 23 Fabio Silva. (Athletic)
Beki wa Everton na Scotland Nathan Patterson anawindwa na Sevilla ambao wanatafuta uwezekano wa kumsajili kwa mkopo. (Liverpool Echo)
West Ham wamekataa ofa kutoka Everton kwa ajili ya kiungo wao wa Kicheki Tomas Soucek mwenye umri wa miaka 30. (Times)
Chanzo cha picha, Getty image
Kiungo wa Brazil wa Fulham Andreas Pereira, 29, ameruhusiwa kuondoka klabuni hapo majira haya ya joto. (Teamtalk),
Wakurugenzi wa Roma watafanya kikao na Liverpool kuhusu usajili wa beki wa kushoto wa Ugiriki Kostas Tsimikas huku Marseille pia wakiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Football Italia), external
Crystal Palace wameingia mbio za kumsajili beki wa kati wa Toulouse Jaydee Canvot, 19, baada ya Aston Villa kukataliwa. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa Bournemouth Philip Billing, 29, yuko tayari kurejea Denmark na kujiunga na Midtjylland kwa dau la pauni milioni 5. (Times),