
Raia wa Togo bado wanasubiri kuundwa kwa serikali mpya, kufuatia kujiuzulu kwa timu ya zamani Mei 2. Kujiuzulu kulikuja usiku wa kuamkia kuapishwa kwa Faure Gnassingbé kuwa Waziri Mkuu ikiwa ni sehemu ya kipindi cha mpito kuelekea Jamhuri ya Tano, ambayo bado inapingwa na baadhi ya vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia. Maandamano mawili ya kuipinga serikali yalifanyika mwezi Juni, na mengine yamepangwa kufanyika mwishoni mwa juma hili.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mawaziri gani watateuliwa tena? Nani atabadilishwa? Hakuna taarifa rasmi ambayo imetolewa kuhusu muundo wa serikali ya baadaye, ya kwanza ya Jamhuri ya Tano, ambayo ilibadilisha Togo kutoka mfumo wa urais hadi wa bunge.
Wakati huo huo, timu inayoondoka imekuwa ikisimamia masuala ya kila siku tangu ilipojiuzulu Mei 2. Kuundwa kwa serikali ni jukumu la Faure Gnassingbé, ambaye alikua Waziri Mkuu siku iliyofuata. Hata hivyo, viongozi wa upinzani wanaeleza kuwa miezi mitatu na nusu baadaye, mawaziri hao bado hawajateuliwa.
Msemaji wa vuguvugu la “Hands Off My Constitution”, Nathaniel Olympio, anaona hii kama ishara ya matatizo katika kuunda serikali mpya. Kwa upande wake, mtaalamu wa masuala ya siasa na mwandishi wa insha Madi Djabakaté anaonyeshea kidole matatizo yanayohusiana na hasira inayotokana na kuendelea kufanyia mabadiliko katiba, hali ambayo ingefanya uajiri wa watu wapya kuwa magumu. “Ukweli ni kwamba serikali ya Jamhuri ya Nne bado iko na inaendelea kufanya kazi,” anaongeza.
Akihojiwa na wenzetu wa Gazeti la Le Point mwezi uliopita, Waziri wa Kazi anayemaliza muda wake, Gilbert Bawara, alibainish kwamba hali hii si mpya wala si ya kawaida, akitoa mfano wa Ubelgiji, ambayo imekuwa na serikali iliyopewa jukumu la kushughulikia shughuli za kila siku kwa zaidi ya mwaka mmoja.