S

Chanzo cha picha, INEC

Maelezo ya picha, Jaji wa Rufani Jacob Mwambegele,

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (INEC) imejikuta katikati ya mjadala baada ya kutangaza kuwa idadi ya wapiga kura katika daftari la kudumu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 imefikia milioni 37.6.

Takwimu hizi zimezua maswali mazito kutoka kwa baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wa haki za binadamu, wakitaka ufafanuzi wa kina kuhusu uhalali wake, hasa kwa kulinganisha na matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Akitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji wa Rufani Jacob Mwambegele, alibainisha kuwa kati ya wapiga kura hao, milioni 7.6 ni wapya, sawa na ongezeko la asilimia 26.55 kutoka idadi ya wapiga kura 29,754,699 waliokuwemo kwenye daftari mwaka 2020.

Licha ya kuwepo kwa ongezeko la vituo vya kupigia kura vinavyofikia 99,911, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 22.49 kutoka vituo 88,567 vya mwaka 2020, mjadala mkubwa umesalia kwenye ongezeko la idadi ya wapiga kura ukilinganisha na watu wenye sifa za kupiga kura kwa mujibu wa Sensa ya 2022, mjadala unaoibua maswali ‘tata’ matatu.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *