s

Katika kile kinachoonekana kama mabadiliko ya upepo wa kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wabunge kadhaa waliokuwa wakitetea nafasi zao wamejikuta wakitemwa na wajumbe wa chama hicho katika kura za maoni zilizofanyika Agosti 4, 2025, katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Ingawa matumaini yao ya kurejea kwenye kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu bado yapo mikononi mwa vikao vya juu vya CCM, uamuzi wa wajumbe unaonesha wazi kuwa baadhi ya majina makubwa huenda yakasalia kuwa historia.

Kada wa siku nyingi wa CCM na Waziri wa zamani, Hamis Kigwangala ameanguka katika jimbo la Nzega Vijijini baada ya kushika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,715. Neto Kapalata ameongoza kwa kupata kura 2,570, nafasi ya tatu imekwenda kwa robert masegere aliyepata kura 1,635.

Katika Jimbo la Vunjo, Dr. Charles Kimei ambaye amekuwa mbunge tangu 2020 ameangushwa na Enock Zadock Koola aliyeibuka mshindi kwa kura 1,999 dhidi ya Kimei aliyepata kura 861. Hii ni mara ya pili kwa Koola kushinda kura za maoni katika jimbo hilo, baada ya kufanya hivyo pia mwaka 2020, ingawa hakupitishwa.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *