d

    • Author, Na Yusuph Mazimu
    • Nafasi,

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza majina ya wagombea ubunge walioteuliwa kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kufuatia vikao vya juu vya chama hicho, ikiwemo Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), vilivyoketi hadi usiku wa manane Julai 28.

Orodha hiyo ilisomwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Amos Makalla, ambapo baadhi ya majina maarufu yaliyotarajiwa kurejea hayakuorodheshwa, jambo lililozua mijadala mikubwa miongoni mwa wanachama na wananchi kwa ujumla.

Miongoni mwa waliokosa kurejea ni kigogo wa siasa na aliyewahi kuwa mgombea urais mwaka 2015, Januari Makamba, jina lake halikurudi katika Jimbo la Bumbuli. Aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini na Naibu Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato jina lake halikurudi.

Waziri wa zamani wa ardhi, Anjelina Mabula jimbo la Ilemela, Naibu Waziri wa zamani wa Michezo, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Pauline Gekul- Babati mjini, na wabunge maarufu Christopher Olesendeka jimbo la Simanjiro, Seif Gulamali wa jimbo la Manonga, pia majina yao yameondolewa.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *