Baada ya Mahakama Kuu ya Gauteng mjini Pretoria kuamua kuwa serikali ya Zambia ina haki ya kuusafirisha mwili wa Rais wa zamani Edgar Lungu hadi nchini mwake, familia yake imejaribu kuwasilisha rufaa ya dharura, lakini ombi hilo limetupiliwa mbali na Mahakama ya Katiba.

Hadi sasa haijajulikani kama familia itarudi Mahakama Kuu ya Gauteng kuwasilisha rufaa kwa utaratibu wa kawaida, lakini Rais wa Zambia Hakainde HichilemaMahakama yaagiza mwili wa Lungu kurudishwa nyumbani kwa ajili ya kuzikwa amesema serikali imewatuma nchini Afrika Kusini maafisa wa Ikulu na wataalamu wa masuala ya kisheria ili kufanya mazungumzo na familia ya marehemu.

Jambo muhimu zaidi ni kwamba tunatarajia kulitatua. Timu yetu ipo pale, wanawashirikisha familia, na msaada wowote ambao unaweza kupata kutoka kwa wanajamii kama ninyi utathaminiwa sana.

Katika hati ya kiapo iliyowasilishwa jana mbele ya mahakama, mjane wa Lungu, Esther Lungu, alisisitiza kuwa maslahi ya haki yanataka kesi hiyo isikilizwe kwa Serikali ya Zambia yafika mahakamani kuzuia mazishi ya Lungu kufanyika Afrika Kusinirufaa ya dharura moja kwa moja. Aliongeza kuwa hakuna mtu mwenye mamlaka ya kulazimishwa kumzika mpendwa wake.

Südafrika Johannesburg 2025 | Messe für den ehemaligen sambischen Präsidenten Edgar Lungu
Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu aliyefariki Afrika Kusini akipatiwa matibabu Picha: Themba Hadebe/AP Photo/picture alliance

Naye Katibu wa Baraza la Mawaziri nchini Zambia, Patrick Kangwa ambaye yuko ziarani Pretoria, amesisitiza kuwa msimamo wa serikali bado haujabadilika, akisema kuwa marehemu Rais anastahili mazishi ya heshima yanayofaa hadhi ya cheo alichoshikilia.

Mwanahistoria na mchambuzi wa siasa za Zambia, Dr. Sishuwa Sishuwa, ambaye kwa sasa anahudumu kama Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Rais wa zamani wa Zambia Lungu afariki akiwa na umri wa miaka 68Historia kwenye Chuo Kikuu cha Stellenbosch Afrika Kusini, amesema mvutano unaoendelea unadhihirisha uhusiano mgumu uliokuwepo kati ya Rais wa zamani, Edgar Lungu, na Rais Hichilema, hasa wakati Hichilema akiwa katika upinzani na baada ya Lungu kupoteza madaraka.

Uhusiano kati ya Lungu na Hichilema ulikuwa mbaya sana, sana wakati Rais Hichilema akiwa katika upinzani na pia baada ya Lungu mwenyewe kupoteza madaraka kwa Hichilema. Wazambia wanashiriki katika uchaguzi wa rais na BungeHivyo basi, mgawanyiko mkubwa unaoonekana sasa ni tu kuendelea kwa asili ya uhusiano waliokuwa nao wakiwa hai.

Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu, alifariki dunia tarehe 5 Juni 2025 wakati akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo mjini Pretoria.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *