
Wakati bado kuna mkanganyiko kuhusu mazungumzo kati ya serikali ya Kongo na waasi wa AFC/M23, ambayo yalianza tena mjini Doha mnamo Agosti 20, diplomasia ya Qatar imevunja ukimya wake siku ya Jumanne, Agosti 26, ili kubainisha kuwa mazungumzo yamekuwa yakiendelea kuhusu mambo mawili: utaratibu wa ufuatiliaji wa kusitisha mapigano na kubadilishana wafungwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mazungumzo kati ya Kinshasa na waasi wa AFC/M23 kwa hakika yameanza tena mjini Doha, Qatar, na pande zote mbili bado ziko tayari kwa majadiliano. Licha ya kusitasita kwa mazungumzo hayo, taarifa hizo zimethibitishwa Jumanne, Agosti 26, na Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, ikitaka kutoa hakikisho.
“Tulipokea hapa Doha pande zote mbili, DRC na M23,” Majed al-Ansari, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar, amesema katika mkutano na waandishi wa habari. Majadiliano yanayoendelea yanalenga “utaratibu wa ufuatiliaji wa usitishaji mapigano, pamoja na kubadilishana wafungwa,” ameongeza, bila kutoa maelezo zaidi.
Idadi ndogo ya wajumbe
Wakiwasili Doha siku ya Jumatano, Agosti 20, serikali ya Kongo na AFC/M23 hadi sasa wametuma wajumbe wachache tu. Wawakilishi wawili kundi kundi hili la waasi walipewa tu jukumu la kujadili mambo mawili yaliyotajwa na Majed al-Ansari kabla ya kuwasili kwa msuluhishi mkuu na timu yake. Kwa hakika, pamoja na ahadi zilizotolewa katika tamko la kanuni zilizotiwa saini Julai 19 zinazotaka kuwezesha kuachiliwa kwa wafungwa kutoka kila upande, mchakato huo bado umekwama kwa sasa.
Wakati huo huo, mapigano yameanza tena kwa kasi, haswa katika mkoa wa Kivu Kusini mwishoni mwa juma lililopita.