#HABARI: Bwana Omary Marcus Msigwa maarufu kwa jina la Super Feo, amechukua rasmi fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi huku akiwaomba wananchi kukichagua chama hicho kwa kishindo kikubwa na kuwaahidi kuchapa kazi kwa ajili ya maendeleo yao kwa kasi kubwa.
Ni wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma, wakimsindikiza mgombea wao wa Ubunge wa imbo la Madaba, Bwana Omary Msigwa (Super Feo) kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Madaba Bwana Abdul Manga.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania