#HABARI: Mgombea Ubunge Jimbo la Mbulu Vijijini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Flatei Gregory, amerejesha fomu ya kugombea Ubunge katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi, huku akieleza hofu yake juu ya njama za baadhi ya watu wanaodaiwa kutengeneza wanachama feki wanaopinga uamuzi wa chama hicho kumteua kuwa mgombea rasmi wa ACT jimbo hilo.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi amesema ana Imani na Tume huru ya Uchaguzi itatenda haki .
Katibu wa ACT Jimbo la Mbulu Vijijini Emmanuel Lenga amesema Uteuzi wa Mgombea wa Ubunge umefuata taratibu zote za chama ili aweze kupeperusha bendera ya chama hicho.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania