#HABARI: Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan, ameambatana na mgombea mwenza wake, Dkt. Emanuel Nchimbi, kurejesha fomu za kugombea nafasi ya urais katika ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) jijini Dodoma Agosti 27, 2025 na tume hiyo kuwateua rasmi kuwa wagombea.
Tukio hilo limehudhuriwa pia na viongozi waandamizi wa chama hicho akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha-Rose Migiro, ambao waliungana na mamia ya wanachama na wafuasi wa chama hicho waliokusanyika kushuhudia tukio hilo muhimu.
Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, ambapo nafasi mbalimbali ikiwemo urais, ubunge na udiwani zitawaniwa na vyama vya siasa vilivyosajiliwa.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania