#HABARI: Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda Maalumu ya Saadani, kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wamefanikiwa kukamata majahazi mawili yaliyokuwa yamebeba zaidi ya magunia 100 ya mkaa, yakiwa yanasafirishwa kinyume cha sheria za misitu kupitia bandari bubu katika bahari ya hindi, ukanda wa Bagamoyo – Chalinze huku watuhumiwa wakikimbia na kuyaacha majahazi hayo katika eneo la Mto Shanga.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania