#HABARI: Watoto wawili wa familia moja Rehema Abeli miaka 3 na Said Abel mwaka 1, wamefariki dunia, baada ya nyumba yao kushika moto wakiwa ndani katika Kitongoji cha Zinduka, kijiji cha Mnyangara, wilaya ya Lindi.
Kwa mujibu taarifa kutoka Jeshi la Polisi mkoani Lindi imeeleza kuwa wakati tukio linatokea, mama mzazi wa watoto hao alikuwa ametoka kuchota maji kisimani umbali wa takribani mita 100 kutoka nyumbani kwake, sasa wakati akiwa njiani kurejea numbani kwake aliona moshi na moto mkubwa ukifuka kutoka kwenye nyumba yao na alipofika alijaribu kuwaokoa watoto wake, lakini alishindwa kutokana na ukubwa na kasi ya moto huo.
Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa ni cheche zilizotokea porini na kurukia kwenye nyumba hiyo, hali iliyosababisha moto kuenea kwa haraka na kuteketeza makazi hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi (ACP) John Imori, ameeleza kuwa uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini undani wa tukio hilo.
Aidha, Jeshi la Polisi limepeleka salamu za rambirambi kwa familia iliyopoteza watoto wake na kuwataka wakazi wa vijiji mbalimbali kuimarisha usalama wa makazi yao ili kuepusha majanga kama hayo huku wakiwataka wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga na majanga ya moto, hasa katika kipindi hiki cha kiangazi.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania