
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amekanusha kwa nguvu zote, madai ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kuhusu kuongezeka kwa vitendo vya chuki na ubaguzi dhidi ya Wayahudi katika nchi yake.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kupitia kwa barua, ambayo rais Macron alimwandikia Netanyahu na kuchapishwa siku ya Jumanne, kiongozi huyo wa Ufaransa, ameonya kuwa, madai ya hayo ya ubaguzi yasitumiwe kama silaha ya vita.
Israel imeishtumu Ufaransa kwa kushindwa kushughulikia kikamilifu matukio ya Wayahudi kushambuliwa, tangu kuanza kwa operesheni yake kwenye ukanda wa Gaza.
Hata hivyo, madai ya Israel kuwa Ufaransa haifanyi lolote, yamekanushwa vikali na rais Macron ambaye amesema hayakubaliki na ni kama tusi kwa taifa hilo la Ulaya ambalo linapanga kulitambua Palestina kama taifa huru ifikapo mwezi Septemba, kitendo ambacho Netanyahu ameonya kuwa, itachochea zaidi kinachoendelea.
Barua ya Macron kwa Netanyahu inakuja baada ya mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani jijini Paris, kujieleza siku ya Jumatu mbele ya Wizara ya Mambo ya nje baada ya Balozi Charles Kushner, kuishtumu Ufaransa kwa kutowachukulia hatua wanaotekeleza mashambulio hayo, madai ambayo Ufaransa imekanusha vikali.