Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, amesema siku ya Jumanne kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda zimekubali kuwarejesha makwao wakimbizi wawalitoroka makazi yao kutonana na mzozo mashariki mwa DRC.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii, iliyotolewa na mkuu wa UNHCR Filippo Grandi mjini Kinshasa, inakuja huku mvutano ukiendelea kati ya DRC na Rwanda, licha ya makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Marekani yaliyotiwa saini mwezi Juni.

Kwa sasa DRC inafanya mazungumzo ya amani na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, ambao wameteka maeneo makubwa ya mashariki mwa DRC.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Rais wa DRC Félix Tshisekedi, Bwana Grandi amesema kuwa wakimbizi 533 wa Rwanda wanaoishi DRC wamerejeshwa Rwanda katika muda wa siku mbili zilizopita, chini ya usimamizi wa shirika lake.

Amezitaka pande zote kuheshimu kanuni kwamba kurejea kwa Wakongo na Wanyarwanda waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia mashariki mwa DRC lazima iwe “kwa hiari.”

Mwezi Juni, shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch lilishutumu M23 kwa kuwafukuza kwa nguvu zaidi ya watu 1,500 nchini Rwanda na kuishinikiza UNHCR kushiriki katika operesheni hiyo, madai ambayo Kigali inakanusha.

Grandi amesema kuwa “hatutaki kile kilichotokia siku za nyuma kijirudi, kama vile ukosefu wa uthibitishaji wa asili ya wakimbizi kurejea makwao kwa hiari.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *