Operesheni hiyo ya siku 15 imefanyika katika Bonde la Baallad, ambapo ndege za Marekani zimefanya mashambulizi mengi huku wanajeshi wa Puntland wakisonga mbele. Kama Africom, Kamandi ya Marekani Afrika, na vitengo vya serikali ya Somalia vya kukabiliana na ugaidi wanadai kuwa wamesababisha hasara kubwa kwa kundi la kigaidi, hakuna hata upande hata mmoja umetoa idadi maalum ya vifo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mapambano dhidi ya kundi la Islamic State (IS) yanaendelea katika Pembe ya Afrika. Siku ya Jumanne, Agosti 26, Africom, Kamandi ya Marekani Afrika, na vitengo vya serikali ya Somalia vya kukabiliana na ugaidi wametangaza kwamba wameendesha operesheni ya pamoja ya siku 15 dhidi ya wanajihadi huko Puntland, kaskazini mashariki mwa Somalia. Ingawa hawakutoa taarifa yoyote ya majeruhi, washirika hao wawili wamejipongeza kwa kusababisha hasara kwa kundi hilo la kigaidi.

Jeshi la wanahewa la Marekani limefanya mashambulizi kadhaa katika Bonde la Baalade, huku wanajeshi wa Puntland wakisonga mbele ardhini. Operesheni hizi zililenga “kuwaangamiza wapiganaji wa mwisho wa ISIS,” vinaandika vitengo vya kukabiliana na ugaidi katika eneo hilo, ambavyo vimekuwa vikifanya kampeni kali dhidi ya kundi hili la wanajihadi katika Milima ya Cal Miskaad tangu mwezi Januari, kwa msaada wa jeshi al wanahewa la Marekani.

Wakati Africom inadai kuwa imefanya takriban mashambulizi zaidi ya arobaini katika eneo hili tangu mwanzoni mwa mwaka, mamlaka ya Puntland inadai kukamata kambi nyingi za wanajihadi.

“Wanajihadi hujificha kwa urahisi”

“Kundi la Islamic State halijashindwa” katika Pembe ya Afrika, hata hivyo, Stig Jarle Hansen, mtafiti katika Chuo Kikuu cha sayanzi za binadamu cha Norway, anaweka mambo katika mtazamo kuhusu Mazungumzo. “Maeneo hayo yanaruhusu wapiganaji kujificha, na wala Adulqadir Mumin [amiri wa kundi] au naibu wake hawajauawa,” anaeleze.

Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Acled, ambalo hukusanya data kuhusu migogoro na maandamano duniani kote, kundi hilo pia limekuwa likitumia ndege zisizo na rubani na vilipuzi vilivyoboreshwa tangu mwezi Januari mwaka jana. ISIS kwa hivyo inaonyesha uwezo wake wa kubadilika kwa “kuongezeka kwa kutumia vifaa zinzopiga mbali,” anasema mtafiti Jalale Getachew Birru, mwanachama wa kundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *