Chama tawala nchini Uganda cha NRM kinafanya Kongamano la wajumbe wake katika ngazi ya taifa leo Jumatano, Agosti 27 na Alhamisi, Agosti 28, mjini Kampala. Tukio hilo kwa mara nyingine litaangazia rekodi ya rais aliyeko madarakani na kumteua kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa urais wa tarehe 12 Januari.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nchini Uganda, chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) kinafanya kongamano la wajumbe wake katika ngazi ya taifa leo Jumatano, Agosti 27 na Alhamisi, Agosti 28, ambapo kitajitayarisha kwa uchaguzi wa urais, ambao utafanyika baada ya miezi minne. Mbali na kuthibitisha uongozi wake, chama hicho pia, katika hafla hii, kitamteua tena rais aliye madarakani, Yoweri Museveni, kukiwakilisha chama chake katika uchaguzi wa tarehe 12 Januari.

Kwa hali hiyo, wafuasi wa Mkuu wa Nchi wanapaswa kuangazia tena rekodi yake: amani, utulivu wa nchi, na, uchumi, Pato la Taifa ambalo limeongezeka mara 17 tangu aingie madarakani mwaka 1986. Rekodi ambayo wapinzani wake wanazidi kutia shaka…

Baada ya kuingia madarakani takriban miaka 40 iliyopita kwa jina la demokrasia na uhuru wa mtu binafsi, Yoweri Museveni hata hivyo amefanya kinyume kabisa, kulingana na mchambuzi huru Frederick Golooba-Mutebi. “Wakati kuna kiwango cha ustawi katika mikoa kadhaa ya nchi, Uganda haijawahi kuhusishwa na vitendo vya na rushwa kama ilivyo leo.” Rushwa mbayo imejikita ndani ya serikali na chama tawala, imeongezeka bila kufikirika na hakuna adhabu yoyote kwa wahusika,” anasema na kuongeza: “Wengi wanabaisha kwamba Uganda ingekuwa na ustawi zaidi na ingefaidika na barabara bora na huduma bora ikiwa tu serikali ya Museveni ingejua jinsi ya kuidhibiti.”

“Rais Museveni ndiye NRM”

Wakati hali ya uchumi ikiwa imezorota, kwa upande wa kisiasa, udhibiti wa rais unasalia kuwa kamili, Frederick Golooba-Mutebi analalamika. “Rais Museveni ni NRM. Anateua uongozi mzima wa chama na kuamua nani atashinda uchaguzi wa ndani ya chama. Ingawa anadai kutoingilia masuala ya chama, sote tunajua anafanya hivyo,” anaongeza.

Ingawa hakatai tathmini hii mbaya, Edward Francis Babu, afisa wa zamani wa NRM, anapongeza hali iliyoko sasa. “Hakika, hali inaweza kuwa bora zaidi, lakini tuna matatizo mengine mengi ya kutatua: hili ndilo ambalo watu hawaelewi,” anabainisha, kabla ya kueleza kwamba rais lazima sasa azungukwe na watu bora zaidi: “Kutawala nchi si rahisi kama inavyoonekana. Yoweri Museveni amefanya mambo mazuri sana na lazima sasa atoe wito kwa timu yenye ufanisi zaidi ili kuipeleka nchi mbele.” Naye Edward Francis Babu anahitimisha: “Tunahitaji kuimarisha msingi wetu, kwa sababu tunajenga kwenye misingi dhaifu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *