Chanzo cha picha, Getty Images
Madaraja ni viunganishi muhimu vya barabara na mito au bahari, na yamekuwa na mchango mkubwa katika kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa na hivyo kuboresha Uchumi na mahusiano ya jamii kwa ujumla .
Katika Orodha hii ya madaraja marefu zaidi duniani tunaangazia madaraja yenye urefu wa muundo wa angalau mita 200 (futi 660). Urefu wa muundo wa daraja ni umbali wa juu zaidi wa wima kutoka sehemu ya juu kabisa ya daraja, kama vile sehemu ya juu ya mnara wa daraja, hadi sehemu iliyo wazi ya chini kabisa ya daraja, ambapo nguzo zake, minara, au nguzo zake za mlingoti hutoka kwenye uso wa ardhi au maji.
Haya ndio madaraja 8 marefu zaidi duniani:
1: Daraja la Huajiang Grand Canyon
Daraja la Huajiang Grand Canyon nchini China limefanyiwa majaribio ya siku tano kabla ya ufunguzi uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa septembaSeptemba.
Jaribio la uwezo wake wa mubeba mizigo ni hatua ya mwisho kabla ya kuchukuliwa kuwa salama kupita juu yake kwa magari ya mizigo. Timu ya kufanya majaribio hayo iliendesha malori 96 kwenye maeneo yaliyoteuliwa ili kupima uadilifu wa muundo wa daraja.
Likiwa na urefu wa mita 625 (futi 2,083) juu ya mto katika mkoa wa Guizhou, daraja hilo likikamilika litaweka rekodi ya kuwa daraja refu zaidi duniani na daraja kubwa zaidi la masafa marefu lililojengwa katika eneo la milima.
2: Millau Viaduct
Chanzo cha picha, Valery Inglebert / 500px
Millau Viaduct au kama Njia ya Millau kwa lugha ya kifaransa Viaduc de Millau ni Daraja lililojengwa kwa Nyaya ambalo lilikamilishwa ujenzi wake mnamo 2004 k . Timu ya wabunifu wa ujenzi wa taraja hilo iliongozwa na mhandisi Mfaransa Michel Virlogeux na Muingereza Norman Foster. Lina urefu wa mita 343 (futi 1,125)
Millau Viaduct ni sehemu ya A75[4]–Njia ya A71 mhimili kutoka Paris kupitia Béziers na Montpellier. Gharama ya ujenzi ilikuwa takriban €Milioni 394 (sawa na Dola za Marekani milioni 424).[2]Ilijengwa kwa zaidi ya miaka mitatu,na kuzinduliwa rasmi tarehe 14 Desemba 2004,
Daraja hilo limeorodheshwa mara kwa mara kama moja ya mafanikio makubwa ya uhandisi ya enzi ya kisasa, na lilipokea Tuzo ya Muundo Bora mwaka 2006 kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa ya Daraja na Miundo
3: Daraja la Çanakkale
Chanzo cha picha, Reuters
Daraja la Çanakkale la 1915 ( au 1915 Çanakkale Köprüsü) ni daraja lililosimikwa katika barabara katika mkoa wa Çanakkale Kaskazini Magharibi mwa Uturuki. Likipatikana kusini mwa miji ya pwani Gelibolu, daraja hilo linazunguka kama kilomita kumi (maili sita) kusini mwa bahari ya Marmara. Ni Daraja refu zaidi la kusimikwa duniani likiwa na urefu wa mita 2,023 (kilomita 2.023; 1.257 )
Daraja hilo lilifunguliwa rasmi na Rais Recep Tayyip Erdoğan tarehe 18 Machi 2022 baada ya takriban miaka mitano ya ujenzi.
4: Daraja la Pingtang
Chanzo cha picha, Getty Images
Daraja la Pingtang ni daraja lililopo katika jiji la Pingtang, Guizhou, China ambalo limebeba Barabara ya Pingtang Luodian iliyopo juu Mto Caodu wenye kina kirefu uliopo bondeni .[
Daraja hilo ni daraja lenye nyaya nyingi na urefu wa futi 7,000 (m 2,100), lina mnara mkuu ambao una urefu wa mita 332 (futi 1,089). Mnara huo ni mrefu ni mfupi tu kwa mita 15 (futi 49) kuliko ule wa daraja la Ufaransa la Millau Viaduct ,
Ni kati ya madaraja 20 ya juu zaidi ulimwenguni na likiwa na barabara mita 310 (1,020 ft) juu ya mto Ujenzi wake uligharimu yuan bilioni 1.5 (sawa na takriban dola milioni 215 za Marekani)
5: Daraja la Mto Husutong Yangtze
Chanzo cha picha, Getty Images
Daraja la Mto Husutong Yangtze ni daraja linalotumiwa kwa safari za Leri na Barabara kwa pamoja ambalo linavuka Mto Yangtze huko Jiangsu, Uchina. Ni kivuko cha reli cha mashariki kabisa cha Mto Yangtze.
Ujenzi wake ulianza tarehe 1 Machi 2014 , lakini likafunguliwa rasmi tarehe 1 Julai 2020.
Kwenye kiwango chake cha juu, hubeba barabara kuu au njia sita kwa za S19 Barabara ya Nantong-Wuxi. Katika kiwango chake cha chini, hubeba njia nne za reli inayosafirisha treni na yenye kasi ya km 200 km kwa saaa , ambayo ilifunguliwa tarehe 1 Julai 2020 . Ina urefu wa mita 1,092 (futi 3,583) na limmeshikiliwa nguzo za minara miwili mirefu ya mita 330 (futi 1,080 )
6: Daraja la Yavuz Sultan Selim
Chanzo cha picha, Getty Images
Daraja la Yavuz Sultan Selim linapatikana nchini Uturuki ambalo pia linajulikana kama Daraja la Tatu la Bosphorus, ni daraja la magari juu ya Bosphorus mlango, kaskazini mwa madaraja mengine ya zamani ya Istanbul ya kusimikwa .
Jiwe la msingi la ujenzi wake liliwekwa tarehe 29 Mei 2013[ na daraja likafunfuliwa rsmi kwa ajili ya safari za magari tarehe 26 Agosti 2016.
Likiwa na urefu wa mita 322 (futi 1,056), ni daraja la 6 kwa urefu duniani.
Pia ni mojawapo ya madaraja mapana zaidi ya kusimikwa duniani, likiwa na upana wa mita 58.4 (futi 192), na kulifanya kuwa mojawapo ya miradi mikubwa zaidi ya usafirishaji.
7:Daraja la Russky
Chanzo cha picha, Getty Images
Daraja la Russky ni Daraja lililokaa kwa nyaya linalopatikana katika eneo la Vladivostok,Primorsky Krai,Urusi. Daraja hilo linaunganisha Kisiwa cha Russky na Muravyov-Amursky Peninsula sehemu za jiji kote, Bosphorus ya Mashariki na mlango wa bahari, .
Likiwa na urefu wa kati wa mita 1,104 (futi 3,622), ni daraja refu zaidi la lililoundwa kwa nyaya duniani.
Mbunifu wa Daraja la hilo ni Russky ni Vlydskinol Ptrov. Daraja la Russky hapo awali lilijengwa kutumika kwa ajili ya ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na pasifiki mwaka 2012 . Ujenzi wake ulikamilishwa mnamo Julai 2012 na kufunguliwa rasmi na na Waziri Mkuu Dmitry Medvedev, na mnamo Septemba 3, 2012, daraja hilo lilipewa jina lake rasmi.
8: Daraja la Sutong Yangtze River
Chanzo cha picha, Getty Images
Daraja la Mto Sutong Yangtze lilibuniwa na Dk. Robin Sham, CBE , FICE , mhandisi wa miundo mzaliwa wa Hong Kong na Uingereza aliyebobea katika ubunifu wa madaraja.
Likiwa na urefu wa mita 1,088 (futi 3,570), lilikuwa daraja lisilo na zenye urefu zaidi duniani kuanzia 2008 hadi 2012.
Minara miwili ya daraja hilo ina urefu wa mita 306 (futi 1,004) . Urefu wa jumla wa daraja ni mita 8,206 (futi 26,923).
Ujenzi wake ulianza Juni 2003, na daraja liliunganishwa Juni 2007 na daraja hilo lilifunguliwa rasmi kwa ajili ya safari tarehe 25 Mei 2008 . Ujenzi umekadiriwa kugharimu takriban Dola za Kimarekani bilioni 1.7.