Makumi ya watu nchini Kenya wametekwa nyara na kuuawa tangu maandamano yalipozuka mwezi Juni 2024

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Makumi ya watu nchini Kenya wametekwa nyara na kuuawa tangu maandamano yalipozuka mwezi Juni 2024

    • Author, Mariam mjahid
    • Nafasi, BBC Swahili

Kusini mwa Jangwa la Sahara imeshuhudia kushuka kwa viwango vya amani katika mwaka uliopita, ambapo wastani wa hali ya amani katika eneo hili ulipungua kwa asilimia 0.17.

Ingawa baadhi ya mataifa yamepiga hatua kuelekea amani, nusu nyingine ya nchi za eneo hili zimeendelea kudidimia.

Kwa sasa, nchi tatu kati ya kumi zenye migogoro mikubwa zaidi duniani zinapatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kulingana na Ripoti ya Amani ya Dunia ya 2025 (GPI), idadi ya migogoro ya kanda imefikia kiwango chake cha juu zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia, na migogoro mingine mitatu iliibuka mwaka huu pekee.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *