Mamlaka ya Rwanda imetangaza siku ya Alhamisi, Agosti 28, kuwasili kwa wahamiaji saba waliofukuzwa kutoka Marekani, ambao wako Kigali tangu katikati ya mwezi Agosti. Hili ni kundi la kwanza kupokelewa chini ya makubaliano ya nchi mbili yaliyotiwa saini mwezi uliopita wa Juni, ambayo yanatoa nafasi ya makazi mapya ya watu 250 waliofukuzwa na Washington.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Majadiliano yamekuwa yakiendelea kati ya Washington na Kigali tangu mwezi Aprili. Walifikia makubaliano mapema mwezi Agosti kwa Rwanda kukubali hadi wahamiaji 250 waliofukuzwa kutoka Marekani. Hata hivyo, Rwanda inabaki na haki ya kukataa kupokea baadhi ya wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani.

Kundi la kwanza la wahamiaji saba waliwasili katika mji mkuu wa Rwanda katikati ya mwezi Agosti. “Wote wamepata msaada ufaao na ulinzi kutoka kwa serikali ya Rwanda,” msemaji wa serikali Yolande Makolo ameliambia shirika la habari la AFP. Miongoni mwao, “watatu kati yao walionyesha nia ya kurejea katika nchi yao ya asili, huku wanne wakitaka kubaki” nchini Rwanda na “kujenga maisha yao huko,” amesema, bila kutaja mataifa yao.

Rwanda, “ina sera nzuri na mapokezi mazuri “?

Na hii ndiyo hoja ya Rwanda katika kutia saini mkataba huu, ambao unajionyesha kama nchi iliyo na mapokezi mazuri kwa wageni. Yolande Makolo alisema mapema mwezi huu kwamba maadili ya jamii ya Rwanda yaliegemea kwenye “kujumuika upya na urekebishaji.”

Wakati huo huo, kundi hili la kwanza, ambalo liliwasili katikati ya mwezi Agosti, linahudumiwa na shirika moja la kimataifa, kwa usaidizi kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na huduma za kijamii za Rwanda, Kigali imeeleza.

Kwa makubaliano haya, Rwanda inakuwa nchi ya tatu ya Afrika kupokea wageni waliofukuzwa kutoka Marekani, baada ya Sudan Kusini na Eswatini. Uganda inatarajiwa kufuata mkondo huo hivi karibuni, baada ya kutia saini makubaliano sawia wiki jana.

Sera hii inaendana na ahadi ya Donald Trump ya kuwafukuza mamilioni ya wahamiaji nchini Marekani wanaoishi kinyume cha sheria, ambao baadhi yao anawataja kuwa “wahalifu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *