Chanzo cha picha, getty
Manchester United wako karibu kufikia makubaliano ya dau kati ya pauni milioni 35 na 40 kumuuza winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 21 Alejandro Garnacho kwenda Chelsea ya Ligi Kuu England (Telegraph)
AC Milan wameingia katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Christopher Nkunku huku mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 27 pia akiwaniwa na Bayern Munich mabingwa wa Bundesliga na klabu yake ya zamani RB Leipzig (Athletic)
Newcastle wanatarajiwa kuwasilisha ofa mpya ya pauni milioni 60 kwa mshambuliaji wa Norway mwenye miaka 25 Jorgen Strand Larsen baada ya awali Wolves kukataa madau mawili ya pauni milioni 50 na 55 awali (Sky Sports)
Kipa wa Paris St-Germain Gianluigi Donnarumma bado hajaondoa matumaini ya kuondoka kabla ya dirisha kufungwa huku Manchester City ikionekana kuwa chaguo bora zaidi endapo kipa wa Brazil Ederson ataondoka klabuni hapo (Sky Sports)
Hakuna mazungumzo yanayoendelea kati ya Al-Nassr ya Saudi Arabia na Manchester City kuhusu Ederson lakini Galatasaray bado wana hamu ya kumsajili kipa huyo mwenye miaka 32 (Fabrizio Romano)
Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham wanamuwinda kipa wa Brazil mwenye miaka 29 John Victor kutoka Botafogo lakini klabu hiyo inataka dau kubwa zaidi ya pauni milioni 6 endapo uhamisho huo utakuwa wa kudumu (Sky Sports)
West Ham wameijulisha Everton kuwa wanataka kumbakisha kiungo wao wa Czech mwenye miaka 30 Tomas Soucek baada ya klabu hiyo ya Merseyside kuonyesha nia ya kumsajili (Athletic)
Tottenham wamekubaliana kumpeleka beki wa Croatia mwenye miaka 18 Luka Vuskovic kwa mkopo wa msimu mzima Hamburg huku kocha Thomas Frank akitafuta kuongeza chaguo jingine kwenye safu ya ulinzi (Standard)
Sunderland wanatarajia kumbembeleza beki wa West Ham na Morocco Nayef Aguerd mwenye miaka 29 ajiunge nao lakini Marseille AC Milan na AS Roma pia wanavutiwa naye (Footmercato)
Manchester City wameijulisha Tottenham kwamba hawana mpango wa kumruhusu winga wa Brazil mwenye miaka 21 Savinho kuondoka msimu huu wa joto hata kama itatolewa ofa zaidi ya pauni milioni 60 (Fabrizio Romano)
Chanzo cha picha, Getty Images
Sunderland pia imewasilisha ofa mpya ya pauni milioni 24 kwa Bologna kwa ajili ya beki wa Colombia mwenye miaka 27 Jhon Lucumi (Sky Sports)
Genoa wanamfikiria Maxwel Cornet wa West Ham baada ya mchezaji huyo wa Ivory Coast kumvutia kocha Patrick Vieira akiwa kwa mkopo msimu uliopita (Tuttomercatoweb)
Kiungo mshambuliaji wa Bournemouth na Ivory Coast mwenye miaka 25 Hamed Traore anatarajiwa kujiunga na Marseille kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua moja kwa moja (Footmercato)
Wolves wanavutiwa na mshambuliaji wa Genk Tolu Arokodare mwenye miaka 24 mshambuliaji wa Nigeria aliyemaliza msimu uliopita akiwa mfungaji bora wa ligi ya Ubelgiji kwa mabao 17 (Sky Sports)