
Baada ya kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea barani Afrika nchini Nigeria, Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote ametia saini kandarasi ya dola bilioni 2.5 nchini Ethiopia siku ya Alhamisi, Agosti 28, kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea katika eneo la Somalia. Mradi huu utaifanya Ethiopia kuwa nchi ya pili barani Afrika kumiliki kiwanda cha mbolea aina ya urea. Nchi hiyo pia inakabiliwa na kupanda kwa bei ya mbolea, athari ya vita kati ya Urusi na Ukraine.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mara nyingine tena, bilionea huyo wa Nigeria anaibuka katika maendeleo na kukuza uchumi barani Afrika. Hii itakuwa mojawapo ya viwanda vitano vikubwa zaidi vya uzalishaji wa mbolea aina ya urea duniani, ikiwa na vifaa vyenye uwezo wa pamoja wa kuzalisha hadi tani milioni tatu kwa mwaka.
Hii ni hatua nyingine muhimu katika mkakati wa upanuzi wa viwanda wa Aliko Dangote, kwani ametia saini makubaliano ya kina na Ethiopian Investment Holdings (EIH), kitengo cha uwekezaji wa kimkakati cha serikali ya Ethiopia, kwa ajili ya maendeleo, ujenzi na uendeshaji wa kiwanda hiki cha hadhi ya kimataifa huko Gode.
Chini ya ushirikiano huu, EIH itashikilia asilimia 40 ya hisa, huku Kikundi cha Dangote kikiwa na asilimia 60 ya hisa katika mradi huo. Gharama ya maendeleo inakadiriwa kuwa dola bilioni 2.5. Uwekezaji huu pia unajumuisha ujenzi wa miundombinu ya bomba la gesi inayolenga kusafirisha gesi asilia ya Ethiopia kutoka hifadhi ya Hilal na Calub hadi kiwanda cha uzalishaji cha Gode, ili kuipatia malighafi.
Soma piaKampuni ya Dangote kutoka Nigeria na Ethiopia kujenga kiwanda cha mbolea cha dola Bilioni 2.5
Ethiopia inakabiliwa na kupanda kwa bei ya mbolea, athari ya vita kati ya Urusi na Ukraine. Kulingana na Bede Heren, mtaalamu wa soko la mbolea wa Argus Media, “uzalishaji wa kiwanda hiki cha baadaye cha mbolea ni tani milioni 3, ambayo inazidi mahitaji ya Ethiopia.” Kwa hivyo itatumika “kusambaza soko la ndani na pia kuuza kwenye masoko ya nje.”
Kwa miaka kumi iliyopita, serikali ya Ethiopia imepitisha mkakati uliofikiriwa vyema kuboresha sekta ya kilimo. Wamekuza shughuli za kilimo, kutathmini hali ya ardhi ili kuelewa vyema ni mbegu gani itafanya kazi katika eneo gani, au ni aina gani itastahimili vyema hali ya hewa ya Ethiopia, kwa mfano. Pia wamezingatia ni mbolea gani itafaa zaidi. Uzalishaji unaotarajiwa wa kila mwaka wa kiwanda hiki cha baadaye ni tani milioni 3, ambayo inazidi mahitaji ya Ethiopia. Lengo la Kundi la Dangote ni, bila shaka, kusambaza soko la ndani, lakini pia kuuza kwenye masoko ya nje. Kwa Ethiopia, upatikanaji wa fedha za kigeni ni tatizo kubwa. Kwa sasa, nchi inaagiza angalau tani milioni 2.5 za mbolea kila mwaka, kwa bei ya wastani ya dola 500 kwa tani. Kwa hivyo sio tu kwamba Ethiopia haitahitaji tena uagizaji huu katika siku zijazo, lakini kiwanda cha Dangote pia kitaleta fedha za kigeni nchini humo.
Kiwanda cha mbolea ni sehemu ya “mkakati unaozingatiwa vyema na serikali ya Ethiopia kuboresha sekta ya kilimo,” anaelezea Bede Heren, mtaalamu wa soko la mbolea kutoka Argus Media.