
Luteni Kelly Ondo, muhusika wa jaribio la mapinduzi dhidi ya rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo Ondimba mnamo Januari 7, 2019, ameachiliwa Jumamosi, Agosti 30. Alikuwa akizuiliwa katika Gereza Kuu la Libreville pamoja na washtakiwa wenzake watatu. Kuachiliwa kwake kumekuja siku moja kama kumbukumbu ya mwaka wa pili wa mapinduzi ya Jenerali Oligui Nguema yaliyomuondoa Rais wa zamani Ali Bongo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Libreville, Yves-Laurent Goma
Akiwa amevalia mavazi meupe, Kelly Ondo amefurahi kuachiliwa uhuru. Walinzi wake wa zamani wa jela waliandamana naye hadi kuachiliwa kwake kutoka Gereza Kuu la Libreville, ambako alikaa miaka sita.
Katika maneneo yake ya kwanza, Kelly Ondo ametoa pongezi kwa wenzi wake wawili waliofariki Januari 7, 2019, wakati jeshi lilipofanya shambulio kwenye kituo cha redio ambapo wanajeshi hao waliojaribu kufanya mapinduzi walikuwa. Hii ilikuwa baada ya kutangaza kunyakua mamlaka.
Alipokamatwa na kufungwa, Kelly Ondo alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.
Baada ya mapinduzi yaliyompindua Ali Bongo mnamo Agosti 30, 2023, sauti zilipazwa zikitaka aachiliwe. Brice Clotaire Oligui Nguema amesema kuwa alacha vyombo vya sheria vifanye kazi yake.
Mnamo Agosti 12, serikali ilipitisha sheria ya kutoa msamaha kwa viongozi wote wa mapinduzi nchini Gabon. Akikejeliwa na watumiaji wa mtandao kwa kuandaa “jaribio la mapinduzi la haraka zaidi duniani,” Kelly Ondo alinufaika na msamaha huu.