#HABARI: Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji George Joseph Kazi, amemkabidhi fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika Ofisi za ZEC, Zanzibar.
Dkt. Mwinyi ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wanachama waliokusanyika kushuhudia tukio hilo muhimu la kidemokrasia.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania #uchaguzimkuu2025