#HABARI: Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bw#HABARI: Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bw

#HABARI: Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bw. Vicent Minja, ameipongeza Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John The Baptist Schools iliyoko Boko Basihaya jijini Dar es Salaam kwa kuunga mkono dhamira ya serikali kuwapatia elimu bora watoto wa kike katika mazingira tulivu.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa TCCIA, Makamu wa Rais TCCIA (Kilimo) Bw. Swallah S. Swallah, ametoa pongezi hizo Agosti 30, 2025 kwenye Mahafali ya 17 yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo, huko Boko Basihaya jijini Dar es Salaam.

“Kazi hii ya kutoa elimu ni kulisaidia taifa la Tanzania kuwawezesha vijana wetu wa kike kupata elimu bora katika mazingira tulivu kama haya.” Alisema.

Alisema, mazingira hayo tulivu yamepelekea mwaka uliopita wanafunzi wote wa kidato cha nne (IV) na sita (VI) kufaulu kwa daraja la I na II.

“Haya ni mafaniko makubwa sana, kwa hiyo ninawaomba wazazi muendelee kuiunga mkono shule hii kwa kuwa mabalozi wazuri, ili hata wale ambao hawafahamu mafanikio yaliyopo hapa wayajue.” Alisisitiza.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *