
“Watu wasiopunguwa 841” wamenyongwa nchini Iran tangu mwanzoni mwa mwaka, Umoja wa Mataifa umesema siku ya Ijumaa, Agosti 29. Ofisi ya haki za binadamu ya shirika hilo imeshutumu “tabia ya utaratibu wa matumizi ya hukumu ya kifo kama chombo cha vitisho vinavyotolewa na serikali.”
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeripoti kwamba kulikuwa na “ongezeko kubwa la mauaji katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025.” “Mamlaka ya Iran imewanyonga watu wasiopungua 841 tangu mwanzoni mwa mwaka na hadi Agosti 28, 2025,” msemaji Ravina Shamdasani amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, akionya kwamba “hali halisi inaweza kuwa tofauti. Inaweza kuwa mbaya zaidi, kutokana na kukosekana kwa uwazi.”
Mnamo mwezi Julai pekee, ameripoti kwamba Iran iliwanyonga watu wasiopungua 110—mara mbili ya idadi ya watu waliopangwa kunyongwa mwezi Julai 2024. “Idadi kubwa ya hukumu ya kifo inaonyesha utaratibu wa kutumia adhabu ya kifo kama chombo cha vitisho vya serikali, na kuzingatia kwa njia isiyo sawa kwa makabila madogo na wahamiaji,” ameonya. Ravina Shamdasani ametaja hasa kunyongwa kwa raia wa Afghanistan, pamoja na Wakurdi wa Iran, Wairan wa Kiarabu, na wanachama wa wachache wa Baloch.
Katika miezi sita ya kwanza ya mwaka, angalau watu 289 waliuawa kwa makosa yanayohusiana na dawa za kulevya. Kulingana na msemaji wa Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, mtindo unaoonekana katika nchi kadhaa unaonyesha kuwa serikali zinazoona upinzani dhidi ya sera zao za kuimarisha usalama zinakuwa kandamizi zaidi na zisizo na uvumilivu.
Kwa mujibu wa makadirio ya mwaka mzima wa 2024, Jamhuri ya Kiislamu iliwanyonga wafungwa wasiopungua 975 waliohukumiwa kunyongwa, idadi ambayo imeongezeka ikilinganishwa na mwaka 2023. Idadi hiyo mpya ya nusu ya kwanza ya mwaka 2025, inazua hofu ya ongezeko kubwa kwa mwaka mzima.
Kunyongwa mbele ya watoto
Ravina Shamdasani alichukizwa hasa na matumizi ya hukumu ya kifo cha umma nchini Iran, huku ofisi ya haki za binadamu ikiwa imeandika watu saba wa aina hiyo tangu mwanzoni mwa mwaka huu, baadhi wakiwa wamenyingwa mbele ya watoto.
“Kunyongwa hadharani kunaongeza safu ya ziada ya hasira kwa utu wa binadamu, sio tu utu wa watu wanaohusika, wale wanaonyongwa, lakini pia wale wote ambao wanapaswa kushuhudia,” amesema. “Maumivu ya kisaikolojia ya kushuhudia mtu akinyongwa hadharani, haswa kwa watoto, haikubaliki,” amesema.
Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuna wasi wasi mkubwa kuhusu mchakato unaotazamiwa katika baadhi ya hukumu za kifo. “Kinachotuhusu hasa ni kwamba nyingi ya hukumu hizi za kifo hutolewa kwa misingi ya sheria zisizoeleweka,” msemaji huyo amesema.
“Adhabu ya kifo haiendani na haki ya kuishi na haipatani na utu wa binadamu”
Ravina Shamdasani amesema kuwa watu 11 kwa sasa wanakabiliwa na adhabu ya “kunyongwa” nchini Iran, wakiwemo sita ambao walishutumiwa kwa “uasi wa kutumia silaha” kwa madai ya uanachama wao katika chama cha upinzani cha People’s Mujahedin cha Iran kilicho uhamishoni. Wengine watano walihukumiwa kifo kwa ushiriki wao katika maandamano makubwa ya mwaka 2022, amesema, akiongeza kuwa Mahakama ya Juu ya Iran ilikubali hukumu ya kifo ya mwanaharakati wa haki za wafanyakazi Sharifeh Mohammadi wiki iliyopita.
“Adhabu ya kifo haiendani na haki ya kuishi na haiendani na utu wa binadamu,” amebainisha. “Inaleta hatari isiyokubalika ya kuwanyonga watu wasio na hatia. Haipaswi kamwe kuwekwa kwa ajili ya vitendo vinavyolindwa na sheria za kimataifa za haki za binadamu,” mwanaharakati huyo amesema.
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Turk, anatoa wito kwa Tehran kuanza kufkiria kufuta adhabu ya kifo.