g

Chanzo cha picha, Jose Chameleone/Facebook

Mahakama mjini Kampala, Uganda, imeahirisha kesi ya talaka
kati ya mtunzi na muimbaji maarufu wa muziki nchini humo Jose Chameleone na
mkewe Daniella Atim hadi Septemba ijayo kutokana na kutoelewana kati ya pande
hizo mbili.

Hii ni moja ya habari zinazogonga vichwa vya habari na kujadiliwa sana nchini
Uganda na miongoni mwa wapenzi wa muziki mkoani humo wanaomfahamu msanii Jose
Chameleone.

Magazeti ya Uganda yanaripoti kwamba Chameleone – majina
halisi Joseph Mayanja, na Daniella, wanatofautiana kuhusu mgawanyo wa mali,
ikiwa ni pamoja na nani atapapewa idhini ya malezi ya watoto, na nani atakuwa mlezi pekee.

Chameleone na Daniella wameoana kwa takriban miaka 17, na
msanii huyo ameimba kuhusu mapenzi yake kwa Daniella katika baadhi ya nyimbo
zake maarufu kwa miaka mingi.

Mwezi Machi mwaka huu, Daniella ambaye sasa anaishi
Marekani aliomba mahakama katika mji
mkuu wa Kampala kumtenganisha na mumewe.

Nyaraka za mahakama zilizonukuliwa na magazeti ya Uganda
zinasema kwamba Daniella anamshutumu Chameleone kwa kutelekeza familia kihisia
kwa miaka mingi, kupuuza majukumu yake, na kushindwa kukidhi mahitaji ya kaya.

Daniella mara nyingi huchapisha kwenye mitandao ya kijamii
matatizo makubwa aliyoyapata katika ndoa yake, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji,
ambao anadai uliutoroka na kukimbilia Marekani kutoroka.

Katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii usiku wa
kuamkia leo, Jose Chameleone alisema kuwa Daniella aliwachukua watoto hao na
kwenda kuishi Marekani kwa ridhaa yao ya pande zote mbili, na kwamba
hakuwatelekeza wala kuacha majukumu yake kama anavyotuhumiwa.

Alisema anataka
kuendelea kupata watoto wake na kwamba popote walipo, atawapelekea kile
wanachohitaji mara kwa mara.

Huku ikisemekana wapendanao hao wa zamani wako katika hali nzuri na kutaka utengano ulioombwa na mke, suala bado liko kuhusu mali.

Magazeti ya Uganda yanaripoti kwamba Daniella Atim anataka kupewa nyumba huko Seguku, kusini mwa Kampala, ulezi kamili wa watoto wao watano, na kwamba Chameleone aagizwe kugharamia matunzo yao.

Chameleone alisikika akisema alikasirishwa na kitendo cha mkewe kumtaka “aonyeshe mambo yake nikiwa bado hai.” Pia alimshutumu mkewe kwa kuwafanya watoto wake wamchukie.

Akasema: “Tunachopigania sio changu ni cha watoto wetu. Na watoto hao watawaachia watoto wao. Tatizo langu wananilazimisha kurithi mali hizi nikiwa hai na mzima.”

Chameleone anadhani yeye na Daniella wanapaswa kutoa huduma ya watoto kwa sababu wote wanafanya kazi.

Mahakama ilisikiliza pande zote mbili na kuahirisha kesi hiyo hadi mwezi ujao.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *