Mahakama ya Rufaa ya shirikisho la Marekani imeamua mnamo siku ya Ijumaa, Agosti 29, kwamba sehemu kubwa ya ushuru wa forodha uliowekwa na Donald Trump haukuwa halali. Rais hawezi kuweka ushuru wa forodha kiholela peke yake. Utekelezaji wa uamuzi huo umesimamishwa hadi mwezi Oktoba. Rais wa Marekani amekata rufaa katika Mahakama ya Juu, ambayo ina majaji wengi wa kihafidhina, ambayo italazimika kuamua.
